Sifa
- Mteja anaweza kustahiki mkopo mmoja tu wa simu unaohusishwa na akaunti moja kwa wakati wowote.
- Huduma hii inapatikana kikamilifu kupitia msimbo wa USSD (*810#) au kupitia programu ya simu ya Caritas Pay.
- Kiwango cha mkopo huanzia Ksh 100 hadi Ksh 70,000.
- Muda wa mkopo ni siku 30, na riba ya kudumu ya 8% hutozwa na kukatwa kabla ya fedha kutolewa.
- Ada ya kuongeza muda wa mkopo (roll-over) ya 8% ya salio iliyobaki itatozwa ikiwa mteja hajalipa ndani ya siku 30; nyongeza hii inaweza kufanyika mara mbili tu.
- Wateja wanaweza kukopa zaidi ya mara moja, mradi hawajafikia kikomo cha juu cha mkopo kilichoidhinishwa (kisichozidi Ksh 70,000).
- Ikiwa mkopo hautalipwa hata baada ya kuongezwa muda (roll-over), mkopo huo utaainishwa kulingana na miongozo ya CRB iliyotolewa na mdhibiti.